Connect with us

General News

Tulikosania mke wangu baada ya kung’ang’ania mtoto wetu

Published

on


PATANISHO: Tulikosania mke wangu baada ya kung’ang’ania mtoto wetu

Bwana Frank alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Irene akidai wawili hao walitengana baada ya mkewe kuondoka kwao bila sababu zozote. Isitoshe sasa mkewe ameanza kupigania mtoto wao.

“Mimi na Irene tumekuwa kwenye ndoa kwa miaka minne, mwezi wa nne mwaka huu aliondoka nyumbani ghafla na kuelekea kwao licha ya kuwa mimi na yeye hatukuwa tumekosana, cha zaidi ni kuwa hata amenipeleka kwa children’s department eti anataka kumchukua mtoto wetu kutoka kwangu” Alieleza bwana Frank akidai, “Ningependa kupatanishwa naye kwa kuwa ni mke wangu na bado ninampenda”

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne.

Aliongeza akisema kuwa ana mke mwingine na anashuku shida ilianza hapo.

“Nilipooa kule Migori, mke wangu naye alikuwa Awendo. Sasa nikiwa na Irene anauliza mbona siendi kumtembelea yule mke mwingine, kumbe alijua kuwa sikuenda maombi ila nilikuwa kwa mke wa pili. ” Aliongeza.

Irene alikatiza mawasiliano yetu aliposkia sauti ya bwanake.

Pata uhondo kamili.

 

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending