[ad_1]
Wajackoya aahidi kuangamiza ufisadi akipata urais
Na SHABAN MAKOKHA
MWANIAJI wa Urais wa Chama cha Roots Party of Kenya (RBK), Profesa George Wajackoya, ameahidi kuwa atahakikisha uchumi wa Kenya unakua kwa asilimia 10 na zaidi iwapo atatwaa kiti cha Urais mnamo Agosti 9.
Ili kutimiza malengo hayo, Prof Wajackoya, alisema kuwa hatavumilia ufisadi na wale wote watakaopatikana kuushiriki, watahukumiwa kifo.Alikariri kauli yake ya awali kuwa akiwa rais, bangi itahalalishwa na kuuzwa nje ya nchi ili kuongezea nchi mapato.
“Ufisadi ni janga ambalo linastahili kutokomezwa nchini kwa njia zote kwa sababu hauchangii ukuaji wa uchumi na nafasi za kazi. Kaunti ambazo zimekataa ufisadi ndio huwavutia wawekezaji,” akasema Prof Wajackoya.
Aliwaomba Wakenya waikatae miungano ya Kenya Kwanza na Azimio inayoongozwa na Naibu Rais Dkt William Ruto na Kinara wa ODM Raila Odinga, akisema kuwa imejaa viongozi wafisadi.
Alikuwa akizungumza nyumbani kwake kijiji cha Indangalasia, Kaunti ndogo ya Matungu, baada ya kuwapokea wanasiasa waliohama vya vingine kisha kujiunga na RBK.
[ad_2]
Source link