Connect with us

General News

Wapinzani wafanya maombi ya pamoja – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wapinzani wafanya maombi ya pamoja – Taifa Leo

Wapinzani wafanya maombi ya pamoja

Na VITALIS KIMUTAI

LICHA ya tofauti zao za kisiasa, Gavana wa Bomet Profesa Hillary Barchok, mtangulizi wake Isaac Ruto na aliyekuwa Waziri Msaidizi wa Madini Dkt John Mosonik, wikendi walijumuika na wakazi wa kaunti hiyo kuombea amani.

Wakati wa maombi hayo, wazee walitakasa uwanja wa Vomet ambao umekuwa kitovu cha makabiliano makali ya kisiasa kati ya wafuasi wa viongozi hao watatu wanaolenga kiti cha ugavana katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Viongozi wa kanisa walimwaga mafuta ya utakaso huku wazee nao wakifanya tambiko na kuutakasa.

Mnamo Januari 10, Naibu Rais Dkt William Ruto alipata mapokezi mabaya katika uwanja huo baada ya wakazi kukataa wito wake kuwa wawapigie kura tu wale wawaniaji wa UDA kwenye nafasi zote kwenye uchaguzi mkuu.

Huku Profesa Barchok na Dkt Mosonik wakisaka tiketi ya UDA, Bw Ruto naye atakuwa akiwania kiti hicho alichopoteza 2017 kwa marehemu Joyce Laboso, kupita chama chake cha CCM.

Wakati wa maombi hayo, wazee na viongozi wa kanisa waliwataka wanasiasa hao waendeleze kampeni zao kwa njia ya amani.

Hata hivyo, hawakuruhusiwa kuhutuba wakati wa hafla hiyo.Kasisi Caleb Langat na Mzee Bartai Milgo walisema maombi hayo ni ya kuombea amani Kusini mwa Bonde la Ufa wakati huu ambapo kampeni zimechacha.

Mnamo Jumanne wiki jana, viongozi hao watatu waliandaa mikutano katika afisi ya Profesa Barchok pamoja na wazee na viongozi wa kidini kisha wakahutubia pia madiwani wa bunge la kaunti hiyo.

Wanasiasa wengine ambao pia walihudhuria maombi ya Jumamosi ni Seneta Christopher Lagat, Naibu Gavana Shadrack Rotich, mbunge mwakilishi wa kike Joyce Korir na wabunge Beatrice Kones (Bomet Mashariki), Gideon Koskei (Sotik), Dominic Koskei (Chepalungu) na Mr Brighton Yegon (Konoin).