Connect with us

General News

Vyama vyataka TSC kuajiri walimu zaidi kumaliza uhaba Tana River – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Vyama vyataka TSC kuajiri walimu zaidi kumaliza uhaba Tana River – Taifa Leo

Vyama vyataka TSC kuajiri walimu zaidi kumaliza uhaba Tana River

NA KNA

WADAU wa elimu katika Kaunti ya Tana River, wametoa wito kwa serikali kutatua uhaba wa walimu eneo hilo ili kuboresha viwango vya elimu.

Afisa wa Chama cha Walimu wa Sekondari na Vyuo (KUPPET), Bw Nelson Oguta, alisema walimu wachache huachiwa jukumu la kufunza idadi kubwa ya wanafunzi, na hivyo kuathiri uwezo wao kuhudumia vyema kila mwanafunzi.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wakuu wa Sekondari (KESSHA) tawi la Tana River, Bw Thomas Mungatana, alisema changamoto hutokana na jinsi walimu wengi ambao si wenyeji huomba kuhamishwa baada ya miaka michache.

Walikuwa wakizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu uliohudhuriwa pia na maafisa wa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC), mjini Hola.Kamishna wa TSC, Bw Mbage Njuguna, alisema ingawa kuna uhaba wa walimu wa shule za upili, hakutakuwa na mapendeleo ya kuajiri wenyeji kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

“Walimu lazima wawe wamehitimu sawa na wengine wa maeneo mengine ya nchi kitaifa. Hatungependa kuwa na walimu ambao hawajafikisha viwango vya ubora vinavyotakikana katika shule zetu,” akasema.

Kulingana naye, kumekuwa na changamoto ya kuajiri walimu wa kutosha kwa sababu bajeti iliyotolewa inaweza tu kuajiri walimu 5,000 kwa mwaka, ambayo ni idadi ndogo mno kitaifa.

“Walimu ambao tunaajiri huwa wanaenda kuchukua nafasi ya wale ambao wamestaafu au wameacha kazi,” akasema Bw Njuguna.

Alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuwepo ushirikiano kati ya wazazi na walimu ili kuboresha matokeo ya wanafunzi shuleni.

“Wazazi wanafaa kusaidia walimu kwa kutoa mandhari bora ya wanafunzi kuhudhuria masomo na pia wawe na ari ya kufuatilia yale ambayo wanafunzi wanafunzwa shuleni,” akaeleza.

Mmoja wa wazazi, Bw Hassan Komora, alilalamika kuwa wakati walimu wanapohamishwa kutoka eneo hili huwa inachukua muda mrefu kabla nafasi walizoachwa kujazwa.