Connect with us

General News

Mwanafunzi ajitosa kwa siasa za useneta wa Kilifi – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mwanafunzi ajitosa kwa siasa za useneta wa Kilifi – Taifa Leo

Mwanafunzi ajitosa kwa siasa za useneta wa Kilifi

NA MAUREEN ONGALA

BAADA ya kugonga vichwa vya habari kama mwanafunzi aliyetimuliwa katika vyuo viwili vikuu nchini miaka michache iliyopita, Bw Fikirini Jacobs sasa ameamua kuelekeza macho yake kwa siasa za uongozi wa kitaifa.

Bw Jacobs, 27, ambaye anataka kuwa seneta katika Kaunti ya Kilifi, alikuwa naibu kiongozi wa muungano wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Maasai Mara (SOMMU), na baadaye akawa kiongozi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Pwani (PUSA).

Akiwa Maasai Mara katika mwaka wa 2017, aliongoza maandamano kupinga mswada wa kurekebisha mfumo wa uongozi wa vyama vya wanafunzi uliokuwa umewasilishwa bungeni na Mbunge wa Garissa Mjini, Bw Adan Duale.

Kulingana naye, msimamo wake kuongoza maandamano hayo ulichangia kutimuliwa kwake chuoni.

“Sheria hiyo haikuwa ya haki na nilisimama kidete kuipinga licha ya kuwa viongozi wenzangu walinitenga. Chuo kilisema, nilikuwa nawachochea wenzangu na nikafukuzwa chuoni kabisa,” akasema.

Baada ya hapo, alijiunga na Chuo Kikuu cha Pwani mwaka wa 2017 akachaguliwa kuwa kiongozi wa wanafunzi.

Alijipata taabani tena alipoongoza mgomo wa kushinikiza chuo hicho kutatua malalamishi ya wanafunzi kuhusu changamoto walizodai walikuwa wanapitia chuoni.Walitaka mandhari ya kimasomo yaboreshwe wakidai kutatizika kwa njia tofauti.

Mnamo Oktoba 14, 2020, Bw Jacobs aliongoza maandano makubwa na kusababisha kutimuliwa katika chuo hicho cha Pwani.Hata hivyo, alirudi katika chuo hicho baada ya mashauriano na kwa sasa anasomea shahada ya filosofia ya sanaa na sayansi ya kisiasa. Bw Jacobs amekuwa miongoni mwa watu wanaopigia debe Chama cha ODM katika Kilifi.

VIWANGO VYA ELIMU

Mzaliwa huyo wa kijiji cha Biyubu kilicho eneobunge la Ganze, Kaunti ya Kilifi, anasema mshawasho wake mkuu kugombea useneta katika kaunti hiyo umetokana na umaskini ambao umewakumba idadi kubwa ya wakazi, na viwango vya chini vya elimu.

“Hatuwezi kuwa tunaenda namna hiyo ndio maana ni lazima tukimbie ili tufikie wenzetu wa maeneo mengine ya nchi,” akasema.Alitoa mfano wa eneo la Bamba, ambapo alidai maisha sio ya kutamaniwa.

“Ni maisha ya uchungu, huzuni na magumu. Kuna ukosefu wa mahitaji ya msingi yakiwemo maji na chakula,” akasema.Hali hiyo ilichangia Bw Jacobs kuja na kaulimbiu ya kuwa ‘Tutafika Pale’ katika kampeni zake.

Bw Jacobs alieleza kuwa, kabla kutaka kuwania useneta, alitaka kuwa diwani wa wadi ya Bamba, lakini akaonelea atakuwa wa manufaa zaidi kwa wakazi wa Kilifi akiwania useneta.

KARISA MAITHA

Alieleza kuwa alipata motisha ya kutaka kuwa seneta kutoka kwa baadhi ya viongozi mfano wa aliyekuwa kiongozi wa watu weusi nchini Amerika, Marcus Garvey aliyejitolea kutetea haki za kibinadamu.

Mpiganiaji haki za binadamu Bw Malcolm X pia amempa motisha ya kupigania jamii yake.Katika bara la Afrika, marais wa zamani Kwame Nkurumah wa Ghana na Robert Mugabe wa Zimbabwe wamekuwa mfano bora kwake kwa misimamo yao ya kutetea haki za Waafrika.

Bw Jacobs aliendelea kusema marehemu Emmanuel Karisa Maitha ndiye kiongozi kutoka eneo la Pwani amempa motisha wa kutaka kuogoza wakazi wa Kilifi.

Pia viongozi wa upinzani wa Africa Kusini, Julius Malema na mwenzake wa Uganda, Robert Kyagulanyi Ssentamu, almaarufu kama Bobi Wine wamemtia nguvu na ujasiri kujitosa katika ulingo wa kisiasa.

Agosti mwaka wa 2014, alipata nafasi ya kipekee ya kukutana na rais Uhuru Kenyatta wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Kilimo katika kiwanja cha Mkomani kaunti ya Mombasa. Rais alimpa tuzo ya kuwa mkulima bora mdogo.